Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi MheDk. Hussein Ali Mwinyi Amepongeza Mashirikiano ya Makubwa ya Taasisi za TAKUKURU na ZAECA
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amepongeza mashirikiano makubwa yanayotolewa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) kwa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA).
Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo Ikulu Jijini Zanzibar wakati alipofanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbungo akiwa amefuatana na ujumbe wake.
Katika mazungumzo hayo, Rais Dk. Mwinyi alisisitiza haja ya kuendelezwa kwa mashirikiano hayo hasa ikizingatiwa kwamba (TAKUKURU) ni Taasisi ya siku nyingi na ina uzoefu mkubwa.
Alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina azma ya kuijengea uwezo hivyo, katika masuala ya uchunguzi, mafunzo na s...