KAMATI YAIPONGEZA TASAF KUSIMAMIA VYEMA FEDHA ZA MRADI
NA ABDI SULEIMAN.
KAMATI ya baraza la wawakilishi yakusimamia Ofisi za Viongozi wakuu wa Kitaifa Zanzibar, imesema imeridhika na utekelezaji wa mradi unaosimamiwa na TASAF Pemba, ya ukarabati wa madarasa Tisa na ujenzi wa ukuta wa skuli ya Piki Wilaya ya Wete.
Kamati hiyo imesema utekelezaji wa mradi huo umezingatiwa viwango bora na vya kisasa zaidi, huku wakiipongeza Tasaf Makao Makuu kwa kuleta fedha na uwezeshaji ambao unatekeleza shuhuli hizo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Machano Othaman Said, aliyaeleza hayo mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea mradi huo na kukagua hali iliyofikiwa, huko Piki Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Mwenyekiti huyo pia ni Mwakilishi wa jimbo la Mfenesini, aliitaka TASAF kuongeza kasi ya uibuaji wa miradi mipya ili kuwasaidia wan...