Bonanza la Michezo kwa taasisi za Serekali lazinduliwa kisiwani Pemba.
YOTE HII NI KASI YA DR. MWINYI ,BONANZA LA MICHEZO LINAWEZEKANA.
Na Maryam Taalib - -Pemba.
MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid amewataka watendaji wa Taasisi pamoja na wananchi kwa ujumla kujenga utamaduni wa kuimarisha afya zao kupitia michezo tofauti ili kuondokana na kupata maradhi hatarishi.
Ameyasema hayo wakati akizindua Bonanza la michezo katika uwanja wa Gombani Kongwe Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba ikiwa ni katika heka heka za kusherehekea kwa kutimiza miaka (60) ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Alisema amefarajika kwa kiasi kikubwa kuona wanataasisi wamejitokeza kwa wingi katika mashindo hayo ya michezo tofauti tofauti.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya alimpongeza Ofisa Mdhamini Wizra ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Pemba M...