Dk. Mwinyi Ameitaka Kamati ya Kuzuia Udhalilishaji wa Kijinsia Zanzibar, iangalie suala la matumizi na athari za mitandao kwa vijana ili serikali ijipange vyema
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameiagiza kamati ya kuzuia udhalilishaji wa kijinsia Zanzibar, iangalie suala la matumizi na athari za mitandao kwa vijana ili serikali ijipange vyema na kwenye mwelekeo wa uhuru wa matumizi hayo kwa Zanzibar.
Dk. Mwinyi aliyasema hayo kwenye hafla ya uzinduzi wa kamati ya kuzuia udhalilishaji wa kijinsia Zanzibar huko ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul Wakili, Kikwajuni Wilaya ya mjini.
Alisema, mitandao inapotumiwa vibaya ni kishawishi kimojawapo cha mmong’onyoko wa maadili na vitendo vya udhalilishaji.
“Naiagiza Kamati hii ifanye kazi ya kuchunguza athari za matumizi ya mitandao ya kijamii na ongezeko la kesi za udhalilishaji, baada ya kufanya kazi hiyo, itoe ushauri na mapendekezo Serikalini ili tuwe na muel...