Dk. Hussein Mwinyi azindua tena Kamati ya Maridhiano baina ya Chama cha Mapinduzi na ACT Wazalendo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameendelea kusisitiza dhamira yake njema ya kuiunganisha tena Zanzibar kuwa moja yenye amani, upendo, maridhiano na mshikamo.
Ameyasema hayo Ikulu, Zanzibar alipozindua tena Kamati ya Maridhiano baina ya Chama cha Mapinduzi na ACT Wazalendo ifanyekazi pamoja kuendeleza amani iliyopo nchini.
Alisema bado ana nia ya kuiendeleza Zanzibar kuwa moja bila kujali rangi, asili, imani za dini, au itikadi za kisiasa kama alivyoahidi kwa mara ya kwanza alipohutubia Baraza la Wawakilishi mwezi Novemba, 2022 juu ya dhamira yake ya kuwaunganisha wananchi wa Zanzibar kuwa wamoja.
Alisema mara baada ya uchaguzi wa mwaka 2020 waliendeleza tena Serikali ya Umoja wa kitaifa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar kama il...