Monday, March 4

Katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ZAC wameandaa majadaliano ya elimu ya Ukimwi.

 

Tukiwa tumo katika maadhimisho ya siku 16 za uanaharakati za kupinga ukatili na udhalilishaji wa wanawake na watoto Leo Afisa Mdhamini Afisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Ahmed Abubakar Ali alikuwa Mgeni rasmi katika majadiliano ya Elimu ya UKIMWI kwa vijana.

Akizungumza na vijana Ahmed amewataka vijana kujitambua na kuthamini utu wao huku wakiwa na uthubutu wa kukataa kurubuniwa na kutumiliwa vibaya katika jamii.

Akizungumzia suala la udhalilishaji mdhamini huyo amesema tukiwa tumo katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga udhalilishaji na ukatili wa wanawake na watoto vijana wanapaswa kuwa tayari kubeba agenda ya kuwekeza katika kuzuwia unyanyasaji na ukatili wa wanawake na watoto huku wakiwa mstari wa mbele kujiepusha kudhalilishana wao kwa wao au kuwadhalilisha wengine na ikitokea hivyo wasiwafiche wale wanaojihusisha na mtendo ya udhalilishaji.