Wananchi wanaombwa kushiriki katika zoezi la uendelezaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura.
PICHA NA BAKAR MUSSA,PEMBA.
BAKAR MUSSA, PEMBA
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Zanzibar,Jaji George Joseph Kazi amewataka wananchi na Viongozi wa vyama vya Siasa Kisiwani Pemba kushirikiana na Tume hiyo katika zoezi la uendelezaji wa Daftari la kudumu la wapigakura linalotarajiwa kuanza tarehe 2/12 mpaka tarehe 15 January 2024.
Akitowa wito huo huko katika ukumbi wa kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba wakati akifungua mkutano wa Wadau wa Uchaguzi Pemba juu ya Tume hiyo kufanya zoezi hilo litakalowawezesha wapiga kura wapya kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao.
Alisema uendelezaji wa Daftari la kudumu la wapigakura linalotarajiwa kuanza katika wilaya ya Micheweni na kumalizika katika wilaya ya Mkoani ni kwa mujibu wa sheria za Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC...